Saturday , 11th Mar , 2017

Meneja wa lebo ya wasanii wa muziki wa bongo fleva ijulikanayo kwa jina la 'Wanene', Gentriez amekanusha kumsajili mkali wa singeli, Man Fongo katika lebo hiyo.

Man Fongo

Hatua imetokana na kuwepo kwa maneno ya chini kwa chini kuwa Man Fongo amejiunga na Wanene, jambo lilifanya eNewz ya EATV kumtafuta Gentrez ambaye pamoja na kukanusha taarifa hizo, pia aliweka wazi kuwa msanii aliyejiunga na Wanene hadi sasa ni Chin Beez pekee.

“Napenda kukanusha kuwa Man Fongo hajasajiliwa Wanene, mpaka sasa hivi ni msanii mmoja ambaye tumemsajili ambaye ni Chin Beez lakini nahisi hizi story zimekuja baada ya kumuona Man Fongo akiwa na bosi wa Wanene katika show ya Ommy Crazy iliyokuwa Tegeta, nahisi ndio maana maneno yamekuwa hivyo". Amesema Gentriez

Pia amesema Wanene kwa sasa haina mpango wa kumsajili msanii mwingine yeyote kwa sasa.

Gentriez