Monday , 9th Mar , 2015

Wasanii wa muziki wa Bongofleva wameendelea kutumia nafasi zao kupaza sauti kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi Albino, kwa kushiriki katika projekti mbalimbali ikiwepo kutengeneza rekodi zenye ujumbe dhidi ya ukatili huo.

msanii wa bongofleva nchini Cassim Mganga

Katika wakati huu ambapo pia jamii ipo katika sintofahamu kwa kuonekana kuendelea kwa unyama huu, eNewz imeongea na Cassim Mganga ambaye ameshiriki katika kampeni ya 'Imetosha' kujaribu kutumia nguvu yake ya ushawishi kukemea na pia kuunganisha nguvu za mapambano dhidi ya hili.