Tuesday , 1st Mar , 2016

Bingwa wa dunia wa riadha ya ndani mita 1500 Abeba Aregawi amefungiwa baada ya kukutwa na vinasaba vya dawa zilizopigwa marufuku.

Raia huyo wa Sweden na Ethiopia alikutwa na hali hiyo alipofanyiwa vipimo na shirikisho la kimataifa la riadha IAAF.

Aregawi, aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya dunia ya Moscow mwaka 2013 na mashindano ya dunia ya ndani ya Sopot mwaka 2014, alikutwa na sampuli B.

Kusimamishwa kwa mwanadada huyo kutafanya aondoshwe kwenye kikosi cha Sweden kitakachoshiriki mashindano ya Olympic mjini Rio Brazil mwezi Agosti mwaka huu.