Friday , 26th Feb , 2016

Kocha wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsène Wenger amethibitisha kuwa nyota Alex Oxlade-Chamberlain ataukosa mchezo muhimu wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester United utakaopigwa Jumapili hii kutokana na kuwa majeruhi.

Winga wa Arsenal Alex Chamberlain akishangila moja ya bao aliloifungia timu yake.

Wenger amesema winga huyo atahitaji kufanyiwa uchunguzi yakinifu baada ya kuibuka hofu kuwa majeraha yatamchukua muda mrefu kupona.

Ushiriki wa Chamberlain kwa Uingereza kwenye kombe la Euro mwaka huu umeshakuwa mashakani baada ya kuumia kifundo cha mguu kwa kukwatuliwa na Javier Mascherano katika mechi ya Arsenal dhidi ya Barcelona mapema wiki hii.

Muingereza huyo ambaye ndiyo kwanza amepata fursa ya kucheza kikosi cha kwanza winga ya kulia, alijitahidi baada ya kuumia lakini alilazimika kutoka mnamo dakika ya 50 wakati Barcelona ikiisambaratisha Arsenal 2-0 Jumatano.

Nyota huyo anaungana na Thomas Rosicky na Santi Carzola ambao ni majeruhi wa muda mrefu msimu huu ndani ya kikosi hicho kinachokamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.