
Wachezaji wakichuana katika soka la Ufukweni
vyuo 12 vya elimu ya juu jijini Dar es salaam nchini Tanzania vimeanza kuchuana katika soka la ufukweni kutafuta bingwa wa michuano inayofanyika kwa mara ya kwanza chini ya usimamizi wa shirikisho la soka nchini TFF.
Mjumbe wa kamati ya soka la ufukweni wa TFF,Joseph Kanakamfumo amesema wameanza na vyuo kutokana na urahisi wa kuwapata wachezaji kutoka vyuoni Kufuatia kuwa tayari kuna uongozi unaosimamia michezo katika vyuo huku baadhi ya vyuo tayari kuanza kucheza soka la ufukweni.
Katika Mchezo uliochezwa mapema leo ,Timu ya chuo cha Teknolojia ya ufundi cha Dar es salaam,DIT kimeinyuka timu ya Chuo cha usimamizi wa Fedha IFM Magoli 5-2,huku sheria na kanuni za mchezo huo zikionekana kuwatatiza wachezaji na hivyo kuathiri ushindani kwa timu hizo.