
Kocha wa man City, Pep Guardiola
Manchestey City, inayoshika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza, nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea, ilizifunga West Ham 4-0 , Swansea 2-1 na FC Bournemouth kwa mabao 2-0 kwa mwezi uliopita.
Guardiola amechukua tuzo hiyo kwa kuwashinda makocha Antonio Conte wa Chelsea, Jose Mourinho wa Machester United, na Tony Pulis wa West Brom.
Naye mshambuliaji wa Tottenham Hospurs Harry Kane, amechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kuifungia timu yake mabao manne katika mechi tatu zilizopita.