
Klopp amesema hayo baada ya mchezo wa jana usiku ambapo Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Swansea. Mjerumani huyo amesema mechi zijazo dhidi ya Leicester City na Burnley watazikosa nyota wake hao.
“Bado tunawakosa nahodha wetu Henderson na Moreno, kuhusu muda wa kurejea sina uhakika ila mechi mbili zijazo za Disemba 30 dhidi ya Leicester City na Burnley Januari 1, hawatakuwepo”, Klopp amewaambia wanahabari.
Ushindi wa jana umeisogeza Liverpool hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa EPL ikizizidi Tottenham Hotspurs na Arsenal. Liverpool sasa ina alama 38 baada ya mechi 20.