
Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa mtoto huyo aitwaye Mofya Lwandamina amefariki jana jioni huko nyumbani kwao Zambia.
“Kwa wana Yanga na wadau wote wa soka, kocha wetu George Lwandamina amepata msiba, amefiwa na mtoto wake wa kiume jana huko Zambia”, imeeleza taarifa ya klabu.
Kocha George Lwandamina ataendelea kuwa kwao Lusaka kwa muda mrefu, ikumbukwe aliondoka Dar es Salaam wiki iliyopita kwenda nyumbani kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanawe wa kike, Nasanta Lwandamina aliyehitimu Stashahada ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha NRDC.
Yanga SC kesho watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kumenyana na Reha FC katika hatua ya 64 Bora ya kombe la shirikisho (ASFC).