Nyota wa Paris St German Blaise Matuid akizungumza na waandishi wa habari.
Akizungumza mara baada ya mchezo Matuidi amesema walicheza chini ya kiwango chao kilichozoeleka jambo ambalo huwa linatokea kwenye timu yoyote hata iwe bora kiasi gani.
Mabao ya Maxwel Cornet na Sergi Darder yaliwapa uongozi Lyon kabla ya Lucas Moura kuifungia PSG bao moja la kufutia machozi.
Kipigo hicho kwa PSG kimefikisha tamati rekodi ya klabu hiyo kucheza mechi 36 bila kupoteza kwenye ligi one ambapo Kwa mara ya mwisho Vijana wa kocha Laurent Blanc kufungwa ni March 15 mwaka jana dhidi ya Bordoux kwa mabao 3-2 .
PSG wanapaswa kushinda mechi tatu zijazo ili kutwaa ubingwa ambao wangetangaza wiki ijayo endapo wangeshinda na Monaco yenye alama 50 wangefungwa au kutoa sare.