Saturday , 26th Jan , 2019

Mjapan Naomi Osaka amemshinda Petra Kvitova wa Jamhuri ya Czech kwenye fainali ya michuano ya wazi ya Australia iliyomalizika mchana huu huko Melbourne.

Naomi Osaka

Naomi mwenye miaka 21 ameshinda kwa seti 7-6 (7-2) 5-7 6-4 na kuchukua ubingwa wa Grand Slams mara mbili mfululizo baada ya mapema mwaka 2018 kuchukua ubingwa wa michuano ya wazi ya Marekani.

Baada ya kutwaa ubingwa huo leo, Naomi sasa ametwaa namba moja duniani kwa wacheza tenisi wa kike kutoka nafasi ya 4 aliyokuwepo kabla ya fainali.

Kwa upande wake Kvitova mwenye miaka 28 ambaye ni bingwa mara mbili wa Wimbledon, yeye ametoka nafasi ya 6 hadi ya 8.

Naomi ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kutoka bara la Asia kushika namba moja huku akiwa ni mcheza tenisi mwenye umri mdogo zaidi kushika nafasi hiyo baada ya Caroline Wozniacki wa Denmark ambaye alikamata namba 1 moja mwaka 2010 akiwa na miaka 20.