Kocha wa Manchester City Manueli Pellegrini
Pellegrini ambaye ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu na kumpisha Pep Guardiola amesema siku zote anaamini kile anachozungumza na ndio maana amekua akifanikiwa kwenye mipango yake.
Kocha huyo raia wa Chile amesema alilaumiwa baada ya kupanga kikosi dhaifu kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Chelsea na kupelekea kupokea kipigo cha mabao 5-1 lakini yeye binafsi alisema aliamua hivyo ili kuwapumzisha wachezaji wake kwa ajili ya kutimiza malengo ya kutwaa mataji waliyoyapa kipaumbele.
Katika Dakika 90 za kwanza, Man City walitangulia kufunga kupitia Luis Fernandinho katika Dakika ya 49 na Liverpool kusawazisha Dakika ya 83 kwa Bao la Phillippe Coutinho na mchezo kuendelea mpaka dakika 30 za nyongeza ambazo zilimalizika kwa sare hiyo
Katika Mikwaju hiyo ya Penati, City walifunga mabao mataty kupitia Jesud Navas,Sergio Aguero na Yaya Toure huku Fernandinho akikosa wakati Liverpool wakifunga kupitia Emre Can na kukosa 3 zilizofuatia zilizopigwa na Lucas Leiva,Philipe Coutinho na Adan Lallana ambazo zote zilichezwa na Kipa wa Willy Caballero.