
C Makonda akiwakabidhi viongozi wa Yanga, hati ya Kiwanja.
RC Makonda amesema eneo hilo lina thamani ya Shilingi milioni 700 ambapo lipo umbali wa Km 14 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere na umbali wa Mita 200 kutoka Barabara kubwa.
Akikabidhi eneo hilo RC Makonda ametaka uongozi wa Yanga kuanza kuliendeleza eneo hilo kwa kujenga uwanja na miundombinu yote inayohitajika.
Wakipokea eneo hilo, viongozi wa Yanga, Bodi ya Wadhamini na mashabiki wa timu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa kuwapa eneo ambalo lipo kwenye mazingira mazuri ya tambarare na kuwatimizia ndoto waliyoishi nayo kwa miaka mingi bila mafanikio.