Thursday , 6th Oct , 2016

Klabu ya Simba SC imeomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wa klabu hiyo katika mchezo wao na Yanga SC wa Oktoba Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mashabiki katika uwanja wa Taifa

Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, kitendo kilichotokea katika mchezo dhidi ya Yanga siyo cha kiungwana na iwapo watagundua ndani ya vurugu hizo kutakuwa na mwanachama wa Simba basi watamchukulia hatua huku wakisema kuwa kwa sasa hawana mpango wa kutafuta Uwanja mbadala ya Uwanja wa Taifa mpaka serikali itakapotoa jibu kuhusu ombi lao la msamaha.

Simba imepigwa faini ya Sh milioni 5 kutokana na mashabiki wake kung’oa viti huku serikali ikivifungia vilabu vyote viwili vya Simba na Yanga kuutumia Uwanja huo kwa muda usiojulikana.