Monday , 3rd Jul , 2017

Timu ya Taifa Stars imeendelea kuonesha mabavu yake katika michuano ya COSAFA baada ya kuwagaragaza wenyeji wao Bafana Bafana bao 1-0, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Royal Bafokeng, Rusternburg usiku wa kuamkia leo.

Stars ilijipatia ushindi huo kupitia mshambuliaji wake Elias Maguri kunako dakika ya 18 na kuifanya timu yake kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia hatua ya nusu fainali ambapo itaenda kuminyana na Zambia siku ya Jumatano ya Julai 5 mwaka huu.

Kwa matokeo hayo mazuri Taifa Stars imeweza kurudisha imani kwa watanzania wapenda soka na endapo wataendelea kucheza kwa uwezo huu, basi kuna asilimia kubwa ya kuweza kufika hata kombe la dunia siku za usoni.