Jengo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kuuli amebainisha hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, baada ya Kamati hiyo kushindwa kufikia muafaka wa kupitisha majina ya wagombea hasa katika nafasi ya urais.
"Kikao chetu cha leo kimefanyika lakini hakijatoa uwaamuzi wa majina ambayo yamepitishwa kutokana na matatizo yaliyotokea jana, mimi kama Mwenyekiti wa kamati nimechukua jukumu na dhamana ya nafasi niliyo nayo kumuandikia barua Katibu Mkuu wa TFF ikiwa dhamira yangu ni kuangalia upya mwenendo mzima wa kamati, nimeshukuru na yeye wamekaa na sekretarieti wamekubaliana na maombi yangu na wameona ni sahihi mchakato huo usimame", alisema Kuuli.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli.
Pamoja na hayo, Kuuli aliendelea kwa kusema " Matatizo yalikuwa mengi na majina ya watu yalikatwa katwa kwa uonevu bila ya kuangalia sifa zao, taratibu zinataka kupindishwa tu kwa sababu ya kutaka kupendelea watu fulani, mimi nadhani siwezi kuwepo sehemu ya kamati ipo namna hii", alisisitiza Kuuli.
Kwa upande mwingine, Kamati ya Utendaji ya TFF imepanga kukutana siku ya Jumanne ya Julai 4 mwaka huu kwa dharura ili kuendelea kuujadili mchakato huu.




