
Mholanzi huyo anafukuzwa baada ya matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England na nafasi yake itachukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na Real Madrid, Jose Mourinho.
Mourinho amekuwa nje ya kazi tangu afukuzwe Chelsea kwa matokeo mabaya pia Desemba mwaka jana.
Pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo zaidi na United kesho na kuna uwezekano akasaini Mkataba wa miaka mitatu pamoja na Rui Faria na Silvino Louro, kocha wa makipa atakaokuwa nao katika benchi la Ufundi.
Taarifa zilienea toka siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa kama kocha wa klabu hiyo.
Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.