Monday , 9th Mar , 2015

Baada ya Simba Sc na bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mashabiki wa Yanga wamewataka viongozi kukaa na kujadili mechi zinazofuata ili kuendelea kufanya vizuri.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Tandale Jumanne Zegege amesema, hivi sasa wanatazamia mechi zinazofuata kwasni wakikaa na kuwaza mechi zilizopita kunauwezekano mkubwa wa kushindwaq kufanya vizuri katika mechi zilizo mbele yao.

Kwa upande wa Klabu ya Simba, Mwenyekiti wa Tawi la Mpira pesa, Ustadh Masudi amesema, mshikamano baina ya viongozi na mshabiki ndio uliochangia timu kuweza kufanya vizuri.

Masudi amesema, mechi ilikuwa ngumu yenye maandalizi na aliyejiandaa kwa ufanisi na uzoefu ndiye aliyeweza kupata matokeo mazuri na Yanga wasijilaumu ila wanachotakiwa ni kukubali matokeo.