
Mbeya City na Yanga
Yanga ambayo mpaka sasa inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 47, inaelekea katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa bao 1-0 na Mbeya City msimu uliopita katika uwanja huo.
Lakini kutokana na muendelezo mzuri wa matokeo ya Yanga msimu huu, ni wazi kuwa Mbeya City watakuwa na kazi ngumu ya kupata matokeo katika mchezo huo.
Yanga imecheza michezo 17 mpaka sasa, ikishinda michezo 15 na kwenda sare michezo miwili huku wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa ukiwa ni 22. Wakati huohuo Mbeya City imecheza mechi 17, ikishinda mechi 6, kufungwa mechi 6 na mechi 5 ikipata sare, ambapo ina alama 23.
Kwa rekodi hizo, Yanga inaonekana kuwa bora zaidi lakini Mbeya City ina faida ya kucheza uwanja wake wa nyumbani, ambapo inaweza kushinda endapo itautumia vizuri.