
Wachezaji na benchi la ufundi la Simba wakishangilia, kulia ni Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.
Akizungumza na www.eatv.tv, Zahera amesema kuwa ubingwa huo haukustahili kuchukuliwa na Simba msimu huu kwa kuwa wamebebwa kwa namna nyingi, jambo ambalo wadau wote wa soka wanalifahamu.
"Ukiniuliza mimi nasema Simba hawakustahili kushinda ubingwa, mambo mengi wamefanyiwa 'fair' na hata wenyewe wanajua na watu wa mpira wanajua", amesema Zahera.
"Mechi nyingi wamebebwa, hata wachezaji wao wenyewe wanakiri suala hilo", ameongeza.
Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu hii leo dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Uhuru, Zahera amesema atakosa huduma ya wachezaji wake 6 ambao wanaugua malaria.
"Maandalizi ya mchezo wa kesho (leo) ni kwamba sitokuwa na wachezaji 6 ambao wote ni wagonjwa, nashindwa kuelewa lakini maandalizi mengine yako vizuri kwa mchezo".