
Baba yake John Woka ametoa taarifa hiyo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa amempoteza mtoto wake na pia jamii imempoteza kijana muhimu.
"Alikuwa ni mtoto wangu wa tatu lakini ni mtoto wa kwanza kwa mama niliyenaye, nasikitika sana kumpoteza kijana wangu, ningependa kuwaambia mashabiki wa John kuwa tumempoteza kijana wetu lakini ni Mungu ndiye aliyepanga na lazima tukubali, msiba utakuwa Ilala Bungoni kwa baba yake mdogo, halafu tutaondoka kwenda Tanga, alafu tutapanga mipango ya kwenda kufanya mazishi", alisema baba wa Marehemu John Woka.
Kwa taarifa ambayo ilitolewa na kaka yake Joni Woka Omari Milay amesem John Woka alifariki alfajiri ya kuamkia leo, katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu, baada ya ajali aliyopata akiwa garage akirekebisha gari.