Thursday , 6th Oct , 2016

Serikali imeanza kuchukua hatua kufuatia kuonekana katika mitandao ya jamii video ya baadhi ya walimu wa shule ya Mbeya Day wakimchangia na kumpiga mwanafunzi wa kiume wa shule hiyo.

Amosi Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala, amesema tukio hilo lilitokea Septemba 28, baada ya mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu kugoma kufanya adhabu ya kupiga magoti na push-up aliyopewa na Mwalimu Frank Musigwa.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mwigulu Nchemba, aliviagiza vyombo vya dola kufuatilia tukio hilo ambapo mkuu wa shule hiyo na baadhi ya walimu wamechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.

Tayari Jeshi la Polisi linawahoji walimu wa shule hiyo huku walimu wanaodaiwa kufanya kitendo hicho, ambao walikuwa shuleni hapo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo wakiwa wamekimbilia kusikojulikana.

Hata hivyo Bw. Makalla amesema kuwa walimu waliohusika na tukio hilo la kumpiga mwanafunzi wamekimbia na vyombo vya dola vinaendelea kuwatafuta ili kuwafikisha mbele ya sheria.

Picha kutoka katika video iliyoonesha walimu wakimpiga mwanafunzi