Thursday , 6th Oct , 2016

Klabu ya Azam FC imesema haijamzuia kiungo Farid Mussa Malick kwenda kuchezea klabu ya Tenerife nchini Hispania bali kuna taratibu zinazotakiwa kufuatwa ndizo zinazomchelewesha kiungo huyo.

Farid Musa alipokuwa kwenye majaribio nchini Hispania

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema, wao kama klabu aliyokuwa akiichezea mchezaji huyo wameshatuma hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwenda nchini Hispania lakini kilichokwama mpaka sasa ni kibali cha kazi cha mchezaji huyo ambacho kinaendelea kufanyiwa kazi na kitakapokuwa tayari ataelekea nchini Hispania kwa ajili ya kuanza kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo.

Winga huyo alifuzu majaribio yake aliyofanya kwa wiki tatu katika mwezi wa Mei mwaka huu na klabu yake iliamua kumtoa kwa mkopo ikikubaliana kulipwa pesa endapo klabu hiyo itamuuza mchezaji huyo kwa timu nyingine.