Friday , 7th Oct , 2016

Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Matthew nchini Haiti inakaribia watu 300 ikiwa ni kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo.

Mwelekeo wa Kimbunga Matthew

Katika Mji wa Jeremie asili mia 80 ya majengo yameporomoka.

Hadhi ya Kimbunga Matthews kwa mara nyingine imepandishwa hadi ngazi ya nne, hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbalimbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Maafisa wa serikali ya haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na maafa yaliyosababishwa na kimbunga hicho.

Kimbunga Matthew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Carebean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.