
Rais John Magufuli
Pamoja na Mambo Mengine wazee hao wamedai kwamba baadhi ya Viongozi wa kuchaguliwa kwa kushirikiana na watendaji Halmashauri ya Monduli wamekuwa wakijimilikisha kinyemela maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi.
Katika Kikao chao kilichofanyika Monduli, wawakilisi wa Wazee hao akiwemo Loti Edward, Melita Laiser na Victoria Nyange wametolea mfano Shamba la Nguvu Kazi katika Kijiji cha Ngarasha lenye ukubwa wa ekari 200 ambalo lilitolewa na Waziri Mkuu wa zaman Hayati Edward Moringe Sokoine kwamba ligawanywe kwa wananchi lakini jambo la kushangaza Viongozi wamejimegea kinyemela.
Aidha Wazee hao wamewashutumu baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kujiidhinishia tenda za ujenzi wa barabara za Wilaya ambazo hata hiyo zimekuwa zikijengwa chini ya kiwango huku wakimwomba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Monduli, Loata Saanare kufikisha malalamiko yao katika ngazi husika.