Friday , 6th Oct , 2017

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki wamesema kuwa wanaimani inawezekana ndugu yao alipigwa risasi kwa sababu ya mambo ya kisiasa ingawa bado wanataka uchunguzi ufanyike ili ukweli kamili udhihirike.

Mdogo wa Mbunge Lissu, Vicent Muhwai Lissu, akifanya mahojiano na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio  amesema ndugu yao alikuwa akikamatwa mara kwa mara kila alipokuwa akifanya shughuli za kisiasa kitu ambacho kinampelekea kuamini kwamba shughuli za kisiasa zinaweza zikawa chanzo cha shambulio la ndugu yao

"Sisi hatujui nini kilipelekea akapigwa risasi lakini mimi ninaamini ni kutokana na mambo ya kisiasa kwa sababu alikuwa akifuata kila alipotoa tamko la kisisasa kesho yake alikuwa akishikwa na kufunguliwa kesi nyingi na zingine za uchochezi ambazo zipo mahakamani na hapo sasa inakuwa rahisi kwa mtu kufikiri kwamba mahakamani ni ngumu anaamua kutafuta,'short cut',  watu waana akili zao wanaweza kufikiria mambo kama hayo. Kama uchunguzi utafanyika basi itajulikana tu ndiyo maana tumesema kwamba wapate msaada kutoka nje ili tuweze kujua"- Amesema  Vicent Mugwai.

Pamjoja na hayo Bw. Vicent amesema ndugu yao amefanyiwa 'Surgery' nyingi na bado anaendelea na zingine lakini wana imani kwamba ndugu yao atapona na atarudi barabarani kuendelea na shughuli zake za kisiasa  kama kawaida.

Pamoja na hayo amesema kitendo cha ndugu yao kugeuzwa mtaji na watu mbalimbali mpaka kufikia kuzungumzia mambo ya ndani ya mgonjwa kinawaumiza kama familia.

Msikilize hapa chini Vicent Mughwai akizungumza zaidi