
Kamanda Haule amesema mtuhumiwa huyo Joseph Dogani alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya marehemu kutaka kuwapiga risasi askari waliokuwa wanamfuatilia.
“Tukio hilo limetokea siku ya Januari mbili majira ya mchana ,Mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha na uvunjaji ,alikuwa anatafutwa kuhusiana na tukio la kujeruhi na kumpora mlinzi silaha aina ya shortgun iliyopatikana baada ya kuuawa kwa jambazi mwenzake”,amesema Kamanda Haule.
Kamanda Haule amesema baada ya kupekuliwa marehemu huyo alikutwa akiwa na bastola yenye risasi nne ndani ya magazine.