
Rais Magufuli akionesha mfano wa Kitambulisho cha wafanyabiashara wadogo.
Kwa mujibu wa Mongela, wamegundua kuna uwepo wa wafanyabiashara Mkoani humo ambao wameanzisha mawakala wa udalali ambao wameamua kuleta makundi ya wafanyabiashara wadogo kuomba vitambulisho hivyo.
Akizungumza kwenye Mkutano wa kugawa vitambulisho maalum kwa wafanyabiashara wadogo, Mongela amesema, "wafanyabiashara ndondogo wanaotetewa na Rais tusiingie mtegoni wa kutumika, tayari tuna taarifa kuna wafanyabiashara wenye uwezo wanaleta makundi ya vijana ili wao wafunge maduka na wapewe machinga wakauze."
Mbali na John Mongela, kiongozi mwingine aliyelia na wafanyabiashara wakubwa kutaka kuchukua vitambulisho hivyo ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri ambaye naye aliwaonya kutofanya kitendo hicho.
Akizungumza kwenye mkutano wa kugawa vitambulisho vya Mkoa huo kwa Wakuu wa Wilaya, Mwanri aliwataka wakuu hao wa wilaya kuhakikisha wafanyabiashara wakubwa hawachukui vitambulisho hivyo.