
Msanii Mimi Mars
Mimi Mars ameiambia Planetbongo ya East Aftrica Radio, kuwa amekuwa akiandika sana ngoma za mapenzi kwasababu ndio kitu ambacho amekipitia na pia marafiki zake wengi wamepitia kwahiyo anajua aandike nini na aache kipi.
''Kiukweli mimi naandika vitu vilivyonizunguka na mapenzi ndio kitu nimekipitia sana lakini haya mambo ya magari sijui pesa kiukweli mada zake ngumu kwasababu sina hivyo vitu tusubiri mpaka nikiwa navyo nitajua vinakuwaje'', amefunguka.
Mimi Mars ambaye ameachia EP inayokwenda kwa jina la 'The Road' yenye nyimbo 6, ameweka wazi kuwa baadhi ya nyimbo haandiki yeye ila anakuwa na stori na idea ya wimbo hivyo anamsimulia mwandishi wake anaandika.
Hata hivyo mwimbaji huyo ambaye amekuwa akiweka wazi kuwa kwasasa hayupo kwenye mahusiano, amekiri kuwa sio kila alichokiimba kwenye ngoma zake kimemtokea yeye kwenye mapenzi bali ni maisha ya kawaida ya kila mtu kwenye mahusiano.