
Prof. Ibrahim Lipumba
Prof Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo, amesema imepita miaka 17 tangu zitokee vurugu hizo hivyo chama hicho kimeona kina sababu ya kuwaombea waliopoteza maisha wakati wakidai demokrasia.
"Maombi hayo ni kwaajili ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha katika vurugu zilizojitokeza mwaka 2001 ikiwa ni baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000".
Maombi hayo yatafanyika katika viwanja vya Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni ambapo maombi hayo yataenda sambamba na ofisi zote za chama kupeperusha bendera nusu mlingoti.