Thursday , 1st Aug , 2019

Afisa Elimu Taaluma Sekondari mkoa wa Arusha Kabesi Kabeja, amepokea kwa furaha msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule za Sekondari Muriet na Kinana.

Akiongea wakati wa kupokea Pedi hizo zilizotokana na kampeni ya Namthamini ya East Africa Television na East Africa Radio, Kabeja ameeleza kuwa ujio wa Pedi hizo utasaidia wanafunzi kujistili na kujiamini zaidi hivyo kuweka bidii kwenye masomo.

"Shukrani zote ni kwenu East Africa Television kwa kuamua kutuchagua sisi kupitia kampeni yenu ya Namthamini, hawa watoto wetu wanapitia changamoto wakati wa hedhi lakini sasa tatizo hilo halipo tena kwa mwaka mzima hivyo wataweka bidii masomoni", amesema.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Muriet Joachim Julius Mdongwe amesema taulo hizo zitawafaa watoto wenye uhitaji.

Kampeni ya Namthamini imewaweka shule kwa mwaka mzima wasichana zaidi ya 300 katika shule za Sekondari Muriet na Kinana.