''Dodoma tulisubiri kwa hamu sana'' - Katambi

Tuesday , 27th Aug , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Patrobas Katambi, ameeleza kufurahishwa na ujio wa kampeni ya Namthamini mkoani humo, ambapo ameweka wazi kuwa walikuwa wakiisubiri kwa hamu sana.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Patrobas Katambi

Katambi ameyasema hayo kwenye zoezi la ugawaji wa taulo za kike katika shule ya sekondari Msalato iliyopo jijini Dodoma, kupitia kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na East Africa Television na East Africa Radio.

''Kampeni hii tuliisubiri sana, niwapongeze EATV na EA Radio kwa kuichagua Dodoma pamoja na kuzunguka nchi nzima kugawa taulo za kike, hakika ni jambo zuri katika kuhakikisha mtoto wa kike anatimiza ndoto zake'', amesema Katambi.

Zoei la ugawaji wa taulo za kike kwa mwaka 2019 linaendelea ambapo tayari mikoa ya Manyara, Arusha na Tabora imeshafikiwa na sasa ni Dodoma, ambapo zoezi hilo limepita katika shule za Hombolo, Kikombo na Msalato na kufanikisha wasichana zaidi ya 500 kusoma bila kupata changamoto wakati wa hedhi kwa muda wa mwaka mmoja.

Zaidi tazama Video hapo chini.