Friday , 13th Dec , 2019

Msanii wa RnB anayewakilisha pande za Morogoro Belle 9, amepata kigugumizi kujibu ni nani mkali kati ya Ben Pol na Juma Jux, ambao wote ni wakali wa muziki wa Rnb hapa nchini.

Katika Picha ni wasanii wa muziki nchini Belle 9, Juma Jux na kulia ni Ben Pol.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Belle 9, amesema wote wawili wapo katika kiwango kimoja na wanafanya kazi nzuri.

"Wote ni wazuri naona wapo katika level moja, wanafanya vizuri, kwangu mimi wote nimefanya nao kazi pia ni watu ambao nina wakubali na ni wadogo zangu maana wamenikuta, lakini kwa kile ambacho wanakifanya nakubaliana nao kabisa hata urafiki wangu kwao ni kwa sababu ya kazi, siwezi kumchana mtu ambaye anafanya vizuri" ameeleza Belle 9.

Aidha Belle 9 amesema kwa sasa ameridhika na amekubaliana na hali yoyote ya maisha itakayotokea kwake.