Wednesday , 15th Jan , 2020

Staa wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amekuwa akisifiwa juu ya utimamu wake wa mwili kwa miaka mingi sasa licha ya umri wake kuzidi kuyoyoma.

Criastiano Ronaldo

Wengi wanataja kuwa mazoezi ndio siri ya mafanikio yake lakini nyuma ya pazia kuna vitu vingi vinavyochangia kwenye utimamu huo wa mwili na kupelekea kulinda kiwango chake mkapa wakati huu.

Ronaldo anatajwa kuwa ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa sana juu ya mwili wake, kuanzia ratiba ya mazoezi, kupumzika, kulala pamoja na lishe. Mshambuliaji huyo mwenye mabao 16 katika mechi 23 msimu huu, anakula jumla ya milo sita kwa siku, huku samaki kikiwa ni chakula anachotumia kwa kiasi kikubwa.

Chakula cha asubuhi, anakula nyama ya nguruwe iliyokaushwa, jibini, na mtindi wenye kiasi kidogo cha mafuta. Chakula cha mchana anakula mara mbili, cha kwanza anakula kuku na saladi na chakula cha pili cha mchana anapenda kula samaki, saladi, mayai na matunda zeituni.

Kabla ya chakula cha usiku anakula matunda freshi na vipande vya parachichi halafu chakula cha kwanza cha usiku anapenda kula samaki na saladi na chakula cha pili cha usiku anakula minofu ya jana 'steak' pamoja na chakula chenye mchanganyiko wa matunda, mayai, unga na nyama iliyosangwa, chakula hicho hujulikana kama 'Calamari'

Inaelezwa pia kuwa Ronaldo anamiliki chumba chenye kimiminika cha Nitrojeni cha kupooza mwili, alichokitengeneza kwa Pauni 50,000 ambapo akisimama kwa dakika tatu anapooza mwili kati ya nyuzi joto 160 na 200.

Kitu kingine kikubwa kinachomsaidia Ronaldo kuwa fiti kimwili ni kutotumia kilevi chochote.