Thursday , 21st May , 2020

Mwanasaikolojia Daniel Marandu amepiga stori kwenye Show ya Dadaz ya East Africa TV, na kueleza athari za mtu mwenye kutegemea hisia ambayo ni mawazo, changamoto, kwenye mahusiano yoyote na atakuwa mgumu kuwa karibu na watu wengine.

Mwanasaikolojia Daniel Marandu

Kwanza ameeleza nini maana ya hisia ambapo amesema  "Hisia ni mihemko ya ndani anayokuwa nayo mtu kuhusu jambo, tukio au mtu mwenyewe, hisia zinasababishwa na unavyofikiria mawazo yako, pia kunaweza kukawa na mihemko chanya au hasi, kama huna hisia basi ujue haujakamilika"

"Athari za mtu mwenye kutegemea kihisia anaweza akapata mawazo, changamoto, kwenye mahusiano yoyote, kwa mfano mwanamke ndiyo anahisia kali kuliko mwanaume, atakuwa mgumu kuwa karibu na watu wengine kwa sababu hawapendi kukosolewa na ukimfanyia hivyo anaweza akakuona adui yake pia hupenda kulaumu watu" ameeleza.