Rosse Ndauka akiwa na mwanaye na mumewe Haffiyy
Rosse Ndauka amesema hayo kwenye show ya Dadaz ya East Africa TV, ambapo ameulizwa kuhusu kubadili Dini baada ya kuolewa na mwanaume wa Kiislam aitwaye Haffiyy.
"Mimi ni Muislam tangu utotoni, mama yangu Muislam na nimekulia katika malezi ya Uislam, japo Baba yangu ni Mkristo na nilikuwa napenda kwenda kanisani, ila baada ya kuwa na mume Muislam nikatoka kwenye Ukristo kuingia kwenye Uislam" amesema.
Msanii huyo wa filamu ameendelea kusema "Upendo ndiyo kila kitu na namshukuru Mume wangu anaupendo sana, hata baba wa huyu mtoto wangu sikuachana nae kwa ubaya na nilipoingia kwenye ndoa alinitumia ujumbe wa kunipongeza".
Zaidi tazama kwenye video hapa chini.