Thursday , 23rd Jul , 2020

Wavuvi na wachuuzi wa samaki zaidi ya elfu mbili katika eneo la Kunduchi pwani waiomba serikali kuu kuingilia kati kuwasaidia baada ya kutakiwa kusitisha kuvua samaki kwa kile kilinachodaiwa kwamba wanatumia nyavu ndogo.

Wakiongea na EATV leo katika eneo hilo wavuvi hao wamesema kwa sasa wanateseka kutokana maisha yao kutegemea kazi hiyo katika katika kujipatia kipato pamoja na kujikimu wao na familia zao.

Wavuvi na wachuuzi hao wa samaki wamesema ni muda wa zaidi ya wiki mbili sasa tangu waletewe barua inayowataka kuacha kuvua samaki kwa kuwa sera ya uvuaji samaki inazuia kuvua samaki kwa kutumia nyavu ndogo.