Wednesday , 2nd Sep , 2020

Ni updates kutoka kwa rapa Khery Sameer Rajab maarufu kama Mr Blue ambaye kupitia post yake aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram amehabarisha kuwa amepata mtoto mwingine na mkewe Waheeda.

Msanii Mr Blue na mkewe Waheeda

"Ahsante mke wangu Mrs Blue Beauty Cosmetics kwa zawadi nyingine alhamdulillah, ahsante sana Mungu kwa kheri zako, karibu sana binti yangu Khairat kwenye familia alhamdulillah, Mungu ni mwema sana" ameandika Mr Blue 

Huyo atakuwa mtoto wa tatu kwa msanii huyo na mkewe kwani hapo awali walikuwa na watoto wawili ambao mmoja wakiume mwingine ni mtoto wa kike.