
Wa pili kushoto Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Pauline Gekul, wa kwanza kulia Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo wakiwa katika ziara katika kiwanda cha Eliya food Overseas Ltd.
Gekul amesema hayo mara baada ya kutembelea kiwanda cha Eliya food Overseas Ltd kilichopo wilayani longido, mkoani Arusha na kupokea changamoto kubwa kutoka kwa wawekezaji hao,kuwa wafugaji wengi bado wanapeleka mifugo yao nchi jirani ya kenya kwa madai ya bei kuwa juu kuliko hapa nchini.
"Wafugaji ifike mahali sasa tuwe wazalendo kwa kuuza mifugo hapa nchini na ifike mahali tujisikie vibaya kunufaisha watu wengine au Taifa lingine, Mifugo itoke Tanzania iende kunuafaisha Kenya, ichakatwe Kenya faida yote iende huko ndugu zangu hapa hatumuungi mkono maana kwa matendo haya kiwanda kinakosa malighafi" alisema Gekul
Aidha Gekul aliahidi kushughulikia changamoto ya wingi wa tozo amelichukua na kuahidi kuwa wizara yake chini ya waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki watakahakikisha kuwa wanaketi na wizara ya fedha kuweza kutengeneza mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji hao.
"Hili la kodi nimelichukua tutakaa chini mapema sana na kuhakikisha tunatatua changamoto hii na niwaombe wafugaji kiwanda hiki kisikose Malighafi,tutakaa chini na waziri wa fedha na Kamati ya bajeti na kushauriana nao,ili mwekezaji huyu wa Elia Food Overseas Ltd atoe bei nzuri kwa wafugaji na wauze mazao hapa" alisema Gekul