
Mshambuliaji Chris Mugalu
Mugalu amepewa kazi ya kuhakikisha anawapa furaha mashabiki wa Simba kwasababu kazi yake ni kufunga na yeye anaijua kazi hiyo.
''Tarehe 6 Januari, 2021 tumempa kazi maalumu Chris Mugalu ya kuwamaliza wajukuu wa Mugabe. Wanasimba tujitokeze kwa wingi kushangilia timu yetu'', Simba wameandika kwenye ukurasa wao wa Instagram.
Mchezo huo utapigwa Jumatano Januari 6, 2021, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Simba SC inahitaji ushindi wa magoli 2 bila wao kuruhusu kufungwa kutokana na kukubali kichapo cha goli 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Harare Zimbabwe.
Katika hatua ya awali, Simba SC iliitoa klabu ya Plateau United ya Nigeria kwa jumla ya goli 1-0 katika mechi mbili, goli ambalo lilifungwa na Clatous Chama kwenye mchezo wa kwanza huko Nigeria kabla ya kutoka 0-0 kwenye uwanja wa Mkapa.