Thursday , 4th Mar , 2021

Dkt Elizabeth Kilili 'mama wa neema' amefunguka kusema yeye alikuwa mhanga wa kutumia mchanganyiko wa vipodozi katika kipindi cha miaka 18 iliyopita hala ambayo ilimletea madhara makubwa kwake, mtoto wake na mumewe.

Picha ya Dkt Elizabeth Kilili akiwa kwenye studio za East Africa Radio

Akizungumzia hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio Dr Elizabeth Kilili amesema

"Nilikuwa muhanga wa vipodozi viambata sumu kwa miaka 18, baadaye viliniletea madhara kwa mtoto wangu akiwa tumboni hadi kwa baba yake pale napokutana nae kimwili au kukumbatiana wakati wa kulala, wakawa wanaharibika ngozi"

"Niliharibika shingo na mgongo, mpaka yale matiti ambayo nilikuwa nanyonyesha mtoto nilikuwa nimepaka mkorogo, sasa zile fangasi zikawa hazimuishi mdomoni mpaka ndani ya utumbo kisha kutokea kwenye choo kikubwa, mume wangu akatupa vile vipodozi nilidata sana kwa kweli maana watu walizoea kuniona nimependeza mitandaoni" ameongeza