Tuesday , 23rd Mar , 2021

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Kimeweka wazi kikosi cha Taifa Stars kitakachosafiiri leo kuelekea nchini Equatorial Guinea kwa ajili ya mchezo dhidi ya taifa hilo wa kuwania nafasi ya kufuzu michuano ya AFCON ya mwaka 2021 nchini Cametroon.

Kiungo wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Said Hamis Ndemla.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha mkuu, Kim Poulsen kimewahusisha wachezaji nyota 30 ambao ni :

Wachezaji ambao wametemwa kwenye kikosi hicho ni Said Hamisi Ndemla, David Charles Manyama, Carlos Protas, Hassan Kessy, Dickson Job, Baraka Majogoro, Ditram Nchimbi, David Bryson na Meshack Mwamita ambao wametemwa kutokana na sababu za kifundi.

Ikumbukwe kuwa, Taifa Stars ipo kundi J, ikiongozwa na Tunisia ambaye amekweisha fuzu akiwa na alama 10, Equatorial Guinea mwenye alama 6, Stars ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 4 huku Libya ikishika mkia ikiwa na alama 3.

Ili Taifa Stars ifuzu kwenye michuano hiyo inahitaji kushika nafasi ya pili kwa kushinda michezo yake miwili iliyosalia dhidi ya Equatorial Guinea wa tarehe 25 Machi 2021 ugenini na ule wa dhidi ya Libya utakaochezwa tarehe 30 Machi jijini Dar es Salaam, Tanzania.