Wednesday , 24th Mar , 2021

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Paul Ince, amependekeza timu yake hiyo kumsajili mshambuliaji mahiri wa timu ya Manchester City Sergio Aguero, pindi atakapomaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Sergio Kun Aguero mfungaji bora wa muda wote wa Man City

Ince kiungo wa zamani wa Man United amesema'' hakuna shaka kwamba Sergio kun Aguero anaweza kuwa jibu la tatizo ya safu ya ushambuliji katika timu ya Manchester United, uhamisho huu nitaufananisha na ule wa Eric Cantona wa mwaka 1992 kutoka leeds''.

Aliongeza kuwa ''Sir Alex Ferguson alifanya maamuzi magumu na ya ajabu kumleta Cantona aliyekuja kumpa faida kubwa ya kufunga magoli 82 kwa misimu yake yote na makombe kadhaa, ikiwemo ubingwa mara 4 wa ligi katika misimu yake 5 lazima Ole Gunnar Solskjael afanye hivi kwa sasa''.

Aguero aliyejiunga na timu ya Manchester City miaka 10 iliyopita akitokea Atletico Madrid ya Uhispania mwaka 2011 anatazamiwa kumaliza mkataba wake 30/6/2021, huku kocha Pep Guardiola akionekana kutokuwa na mpango wa kumuongezea mkataba kutoka na majeraha ya mara kwa mara na katika msimu huu amecheza mechi 8 tu za ligi kuu.

Uhamisho huu ukifanikiwa itakuwa kama ajabu kwa sababu timu hizo zinazotoka katika jiji moja la Manchester hawana tamaduni za kuuziana au kubadilishana wachezaji tangu zama hizo ni aghalabu kutokea, japo Man United wanaweza kunufaika na kuwa huru kwake baada ya mkataba kuisha.

Aguero ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo tangu amejiunga mwaka 2011, amefunga magoli 257 katika mechi 384 za mashindano yote aliyocheza.