
Paul Makonda, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Kauli hiyo ameandika hii leo Machi 25, 2021, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ikiwa zimepita saa kadhaa tu tangu ashiriki kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, mkoani Mwanza hapo jana.
"Pamoja na kukuona jana bado moyo wangu unaamini umelala hujafa, rafiki, kaka na kiongozi wangu utakapoamka usingizi kuna jambo nitakwambia," ameandika Makonda.
Hayati Dkt. John Magufuli, alifariki dunia Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na atazikwa kesho Machi 26 kijijini kwao Chato.