
Karim Benzema akishangilia moja ya magoli yake
Benzema ambaye yupo kwenye kilele cha mafanikio yake kwa sasa, amekuwa mhimili mkubwa sana wa klabu ya Real Madrid tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo aliyetimukia Juventus ya Italia, na hivyo jukumu la kufunga kuachiwa yeye.
Katika msimu wa mwaka 2019/20 Benzema alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu kwa wachezaji raia wa Ufaransa, ambapo alimaliza msimu wakiwa mabingwa wa La Liga, akichangia kwa mabao 21 na pia msimu huu wa 2021/22 ameanza vyema sana ikiwemo kuifanikisha timu yake kuingia katika hatua ya robo finali ya klabu bingwa Ulaya.
Mashabiki wamegawanyika katika pande mbili, wapo wanaomuunga mkono msimamo wa kocha wao Deschamps kutomjumuisha katika timu ya taifa, huku upande mwingine ukipinga msimamo huo wakitaka ajumuishwe kutokana na ubora wake wa sasa hasa kuelekea katika mashindano ya Euro 2021.
Licha ya kuwa katika kiwango bora kwa misimu mitano mfululizo, Benzema hajajumuishwa katika timu hiyo kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu akihusishwa na mchezaji mwenzake wa wakati huo Mathieu Valbuaena.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa vyanzo na mifumo tofautitofauti umeonesha 55% wanahitaji kumuona tena Benzema katika jezi ya bluu akisaidiana na nyota wao mpya Kyllian Mbappe katika safu ya ushambuliaji.
Katika msimu huu Benzema amefunga magoli 17 katika michezo 24 ya La liga, amefunga pia magoli 5 katika michezo 6 ya klabu bingwa Ulaya na goli 1 katika kombe la mfalme na kumfanya awe amefunga jumla ya mabao 23 hadi sasa na msimu ndiyo bado.