Thursday , 29th Apr , 2021

Wanandoa wawili Imelda Augustino (30) na mume wake Augustino Mushobozi (37) wakazi wa Mubunda tarafa Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera, wamepoteza maisha baada ya mume kumkatakata kwa kitu chenye ncha kali mke wake na kisha naye kujiua kwa kwa kujinyonga kwa kutumia chandarua.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kagera Maketi Msangi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 25 mwaka huu saa mbili usiku,  na kwamba baada ya baba huyo kumuua mke wake alikwenda jirani na makazi ya Sued Kabakama na kujitundika juu ya mti kwa kutumia kipande cha chandarua.

Kaimu kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro kwa wanandoa hao ambapo mume alimtuhumu mke wake kuwa ana mahusiano nje ya ndoa.