Saturday , 8th May , 2021

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limasogeza mbele mchezo wa Ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga kutoka Saa 11:00 Jioni na sasa mchezo huu utachezwa Saa 1:00 Usiku katika Dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Mshambuliaji wa Simba SC Luis Miquissone (kulia) akiwatoka wachezaji wa Yanga SC

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF imesema kuwa imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mchezo huo kutoka Wizara ya Habari, Utamadubi, Sanaa na Michezo.

 Taarifa ya TFF