Tuesday , 1st Jun , 2021

Sean Kingston anarejea na album mpya ‘Deliverance’ siku za hivi karibuni baada ya miaka 8 kupita tangu atoe album yake ya mwisho Back 2 Life mwaka 2013 na tayari ameachia wimbo wa kwanza ‘Darkest Times’.

Picha ya Sean Kingston

Mmiliki huyo wa hits kama ‘Beautiful Girls na Eenie Meenie’ ameeleza kuwa ujio wa album hii ya nne utarejesha mahusiano yake na mashabiki wake ambayo yalikuwa yamefifia kutokana na kukaa kimya kwa zaidi ya miaka 8.

Mkongwe huyo aliwahi kufanya kazi na wasanii wenye majina makubwa kwenye muziki kama Trippie Redd, Bow Wow, Brandy, Flo Rida, Chris Brown, Sean Paul na Nicki Minaj huku akijigamba kuwa sauti yake haijabadilika sana na bado anaishi kwenye mizizi yake yenye nguvu ya Jamaika.