
Kocha wa Namungo, Hened Suleiman Morocco akitoa maelekezo akiwa benchini.
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Namungo, Hemed Suleiman Morocco amesema licha ya Prisons kuwa timu ngumu na wapambanaji lakini wanauhitaji mkubwa wa matokeo mazuri katika mchezo huo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Morocco amesema, “Tunashukuru mwenyeenzi Mungu tupo vizuri, ni mechi nyengine ngumu kwetu sisi tunacheza na Prisons, wapo vizuri na ni wapambanaji lakini naamini kwanza tunahitaji kushinda mechi ili tuwe kwenye mazingira mazuri”.
Katika kujibia namna mchezo huo utakavyokuwa kiupinzani, Morocco amesema, mchezo huo utakuwa wa aina yake hii leo.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu ofcourse wana uzoefu mkubwa katika Ligi na sisi tunajipanga kupata matokeo nafikiri itakuwa mechi ya aina yake”.
Kwa upande wa TZ Prisons, watahaha kusaka alama tatu ili kujiondoa kwenye hofu kabisa kwenye hatari ya kushuka daraja.
Namungo ipo nafasi ya 8 ikiwa imecheza michezo 29 na kujizolea alama 40 utofauti wa alama 5 na timu ya Biashara United Mara inayoshika nafasi ya 4 yenye alama 45 ilhali TZ Prisons ipo nafasi ya 7 ikiwa na idadi sawa ya michezo na alama na Namungo.