Wednesday , 2nd Jun , 2021

Ukurasa wa instagram wa lebo ya Kings Music umemtaja msanii Alikiba kama ndiye True Swahili Nation na The Greatest of all time (GOAT) kwani tangu ameanza muziki hajawahi kutumia vionjo vya muziki mwingine tofauti na Bongo Fleva na bado yupo kwenye ubora wake.

Msanii Alikiba

"Hajabebwa na international collabo, hajatumia Niger flavour wala amapiano, hajatumia vionjo vya Amerika, hana janja janja, hafanyi kiki,hatii huruma zaidi ya kusimama na muziki wake na mashabiki zake na wala hatumii nguvu kubwa ku-push kazi zake lakini anashinda Tuzo za kimataifa na anafanya shows za kimataifa halafu yupo on top kwenye game miaka 18 sasa hajawahi kushuka wala kuchuja ndio maana anaitwa mfalme wa muziki Afrika".