Monday , 19th Jul , 2021

Zoezi la uchangiaji wa taulo za kike na pesa kwenye Kampeni ya Namthamini ili kuwasaidia wanafunzi wa kike kubaki shule mwaka mzima limeendelea Julai 17 Shoppers Supermarket Mlimani City ambapo watu wengi wajitokeza kuchangia.

Mwanamke Kinara Maryam Kitosi kulia, Flaviana Matata kushoto

Team nzima ya East Africa Television, East Africa Radio kushirikiana na Flaviana Matata Foundation chini ya mwanamitindo maarufu Flaviana Matata walikuwepo kukusanya michango hiyo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Na wewe pia unaweza kuwasilisha mchango wako kwa kuleta ofisi za East Africa TV Mikocheni au kutuma pesa kupitia mtandao wowote wa simu, lipa kwenda namba 5999900 jina ni East Africa Television.

#Namthamini #NasimamaNaye